Mambo 6 ya Kuzingatia Ukiwa na Bosi Uliyemzidi Umri Kazini

  | 3 min read
0
Comments
2395
bosi mdogo

Katika kizazi hiki cha wafanyakazi wenye umri tofauti tofauti, makampuni mengi huamua kuajiri au kuwapandisha vyeo wafanyakazi wenye ujuzi na wenye uwezo mzuri kikazi kuwa wasimamizi. Hii inaweza kupelekea wewe kuwa na Bosi uliyemzidi umri na huenda usifurahie kazi yako kwa sababu ya umri wa bosi wako. Utafiti unaonyesha kwamba wafanyakazi katika makampuni yenye mabosi wenye umri mdogo kuliko wao huwa na hisia hasi ikilinganishwa na wale walio na mabosi waliowazidi umri.

Ikiwa wewe na meneja wako mheshimiana, kufanya kazi pamoja haipaswi kuwa tatizo. Ni muhimu zaidi kuzingatia ukuaji wa kazi yako kuliko kuhangaika juu ya umri mdogo wa bosi kazini kwako. Hivi ni vidokezo unavyopaswa kufikiria ili kufurahia kufanya kazi na meneja uliyemzidi umri.

1. Wape Heshima Wanayostahili

younger manager older employee

Bosi wako anaweza kuwa na umri mdogo kuliko wewe, lakini hii haimaanishi kwamba hana uwezo unaotakiwa. Ni muhimu kusikiliza na kuheshimu maamuzi yao. Hii inamaanisha kwamba mambo ambayo utafanya ili kuonyesha heshima kwa bosi wako wa zamani hayana tofauti na kwa bosi mwenye umri mdogo kwako. Kubali kuwa yeye ni mtu sahihi kufanya kazi hioyo na daima kuwa muwazi kwa mawazo anayoleta na kukubali kwa mtazamo chanya. Ikiwa unaonyesha heshima kwa bosi wako, ni wazi kabisa kuwa utaipata ya kwake kwa urahisi pia.

2. Tumia Uzoefu Wako kwa Hekima

Uzoefu wako katika kufanya kazi katika kampuni hiyo ni moja ya zana muhimu zaidi ambazo unaweza kutumia katika kuimarisha uzalishaji na ufanisi wa shirika. Unaweza kutumia hii kumsaidia bosi wako mdogo kukuza ujuzi wake katika kuongoza timu na kusaidia kampuni kukua. Bosi wako anaweza kuwa na ujuzi katika eneo fulani kama vile teknolojia lakini hajui mengi kuhusu mawasiliano. Unapaswa kuwa tayari kumfundisha ujuzi uliyopata kwa miaka mingi na atatambua mchango wako kwa kampuni kirahisi zaidi kwa ukuaji bora wa kazi yako baadaye.

3. Kuwa Tayari Kubadilika na Kujifunza

older workers younger managers

Kuwa tayari kubadilika kuhusu namna mambo yanavyofanyika katika ofisi ni muhimu. Bosi wako anaweza kuchagua njia tofauti ya kutatua matatizo katika kampuni. Kizazi cha vijana kinasemekana kupenda teknolojia zaidi kufanyia kazi, hivyo unaweza kuhitaji kubadilika na kujifunza ufanane na kasi ya bosi wako. Makampuni mengine hufanya kazi na watu katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Kwa hivyo bosi wako anaweza kuchagua mitandao kama vile Slack kwa mawasiliano. Daima kuwa tayari kukubali changamoto mpya kama hizi.

4. Usiumize Kichwa Sana

Kazi na maamuzi uliyofanya katika kazi zako ndio yamekusaidia uwe katika nafasi yako ya sasa. Uko katika nafasi hii kwa sababu ya kazi yako na kwamba unapaswa kujivunia. Hutakiwi kufikiri kwamba timu ya uongozi inakuona kuwa duni zaidi kwa sababu walitoa jukumu la ubosi kwa mtu mwingine aliye mdogo kuliko wewe. Kuwa na ujasiri kukubaliana na ukweli kwamba walikuajiri ili kuleta thamani maalum kwa timu. Hakikisha unajaribu kufanya kazi na bosi wako mdogo na kujitoa kwa kila ulicho nacho kufanikisha kazi hiyo.

5. Mawasiliano ni Muhimu

working for younger manager

Mawasiliano ya wazi kati ya wewe na bosi wako yatawafanya muweze kuelewana na kujenga mazingira mazuri ya kazi. Tafuta njia yake nzuri ya mawasiliano ili kuunda mazungumzo sahihi, kujenga imani na kuboresha tija ya kampuni.

6. Zingatia Ukuaji wako wa Kazi na Kampuni

Mwisho, unapaswa kukumbuka kuwa upo katika nafasi uliyopo kama ulivyokusudia waukianza kazi yako. Daima amini kwamba kazi yako itaendelea kukua bila kujali tofauti ya umri kati yako na bosi wako. Kwa kuongeza, kumbuka kwamba wewe na bosi wako mpo kwenye timu moja na lengo lenu ni moja, kukuza kampuni.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media