Uajiri wa Wahitimu: Kwanini Uajiri Wahitimu Wapya

  | 4 min read
0
Comments
744

Wahitimu watapata vipi uzoefu kama kila mtu hataki kuwaajiri

Moja ya vikwazo vikubwa katika kutafuta kazi kwa wahitimu ni kuona maelezo ya kazi amabyo wanajua wanaweza kufanya lakini miaka ya uzoefu inayohitajika inawazuia kuomba kazi. Ingawa kazi nyingi za daraja la kati na juu zinahitaji mtu ambaye ameshafanya kazi kwenye soko kwa muda fulani, kazi za daraja la chini hazihitaji mtu mwenye uzoefu wa miaka 3 paka 5!

Kwanini waajiri hufanya hivi?

Jibu ni rahisi, hawataki kuajiri wahitimu waliomaliza tu chuo.

Tanzania, kuna mtazamo mkubwa kati ya waajiri kuwa wahitimu wa chuo hawafai kwa sababu:

 •       Watahitaji mafunzo mengi
 •       Wanaweza wasijue tabia zinazokubalika mahala pa kazi
 •       Watahitaji usimamizi mkubwa
 •       Hawana uwajibikaji

Ingawa vijana wana hasara zao kwenye ajira, kuna faida nyingi zaidi kuliko hasara ambazo mwajiri atapata kwa kuajiri wahitimu. Hizi hapa faida 10 amabazo utazipata kwenye biashara yako kwa kuwekeza kwa wahitimu wapya.

 1. Wana ari ya kuonyesha kuwa wanaweza

Hakuna kundi lilioathiriwa na ukosefu wa ajira kama wanafunzi wa chuo, taarifa zinaonyesha kiwango cha ukosefu wa ajira ni zaidi ya 14% katika vijana wa umri wa miaka 18 paka 24. Hivyo wahitimu wengi hujikuta wakikaa miaka mingi bila kazi. Hii inamaanisha watakapopata kazi, watakuwa na ari ya kuonyesha juhudi zaoili kuthibitisha kuwa wanastahili kazi hiyo.

 1. Wana ari ya kujifunza

Kwa watu wengi, kadri umri unavyosogea, ndio hamu ya kujifunza vitu vipya inapungua. Wahitimu wapya wa chuo wana akili changa ambazo ni rahisi kufundishika na  kupokea ujuzi mpya, na kwa sababu hawana uzoefu wa kazi, wanakuwa wapo tayari kufundishwa na watu wenye uzoefu mkubwa zaidi yao.

 1. Wanajua teknolojia

Wahitimu wapya wa chuo wamekua katika nyakati za mabadiliko makubwa ya kiteknolojia, na wanakuwa na uwezo mkubwa wa kutumia vifaa vya kielektroniki na programu mbalimbali. Hutohitaji kuwafundisha namna ya kutumia kompyuta. Na wanaweza hata kusaidia kutatua baadhi ya matatizo madogo ya IT, kuweka programu muhimu kwenye vifaa mbalimbali, na kukupa dondoo za teknolojia zitakazo saidia utendaji kazi.

 1. Wana gharama nafuu

Hili lipo wazi, mhitimu yoyote atakubali mshahara mdogo kuliko mtaalamu mwenye uzoefu kwenye soko tayari. Kama unajaribu kubana matumizi, hii itakusaidia kuboresha bajeti yako.

 1. Wana mitazamo mipya kuhusiana na mambo mbalimbali

Kama umekuwa katika mazingira yaleyale kwa muda mrefu, inakuwa ngumu kupata mawazo mapya. Lakini mtu mpya akiingia kwenye mazingira hayo anaweza kuona kitu ambacho wewe umeshindwa kukiona. Pamoja na kuleta mitazamo mipya, wahitimu wanakuja na maarifa na ujuzi mpya waliojifunza chuo mabao unaweza kusaidia kampuni yako.  

Pia kwa sababu hawaja wahi kufeli kwenye kazi na hawajawahi kukutana na ukiritimba wa kazini, itakuwa ni rahisi kwao kuwasilisha na kujaribu mawazo mpya kwenye utendaji kazi wao.

 1. Utayari wa kufanya kazi masaa mengi na kusafiri

Fani kama za ushauri, benki za uwekezaji na utangazaji zimeanza kugundua  faida za kuajiri vijana waliohitimu, mara nyingi wanakuwa hawana familia nyumbani, hivyo wako tayari kutumia muda wao binafsi kufanya kazi. Hii inawafanya wafiti kwenye ajira zinazohitaji kusafiri mara kwa mara na zenye masaa mengi ya kazi.

 1. Wanaelewa mienendo ya mtandaoni

Katika enzi hizi, kila biashara itahitaji kurekebisha mikakati yake ili kuweza kupata wateja wa mtandaoni. Zaidi ya 40% ya Watanzania wana umri chini ya miaka 25, bishara zinahitaji kujua ni njia gani zitumie ili kuvutia vijana mtandaoni. Wahitimu wapya vijana, pamoja na kutumia intaneti wenyewe, pia ni sehemu ya soko hili la mtandaoni na hivyo wanaweza kuchangia mawazo kwenye mikakati ya kuvutia wateja mtandaoni.

Mfano, mhitimu mpya anaweza kukwambia ni chapisho lipi ka Instagram linavutia zaidi, litakalo vutia watu wengi zaidi.  Wanaweza kukupa mawazo kuhusu kutangaza YouTube. Na siku zote watakua wanajua ni app ipi, au tovuti ipi ambayo ndio maarufu zaidi, hivyo kusaidia biashara yako kuongoza kwenye soko.

 1. Watakufanya uwe bosi mzuri

Utajifunza mengi kuhusu kuwa bosi mzuri kwa kufanya kazi na vijana. Wanapendelea:

 •      Kupokea vizuri maoni yanayo wakosoa na kujirekebisha
 •      Wanapata motisha kubwa zaidi kwa kupata maoni mazuri kushinda hata bonasi za fedha
 •      Wanafuatilia uongozi kwa karibu, na wanafadhaika pale maneni ya bosi wao yasipofanana na vitendo
 •      Wanapendelea kutafuta mtu wa kuwafundisha mwenye uzoefu zaidi yao

Kiujumla vijana ni kundi ambalo utendaji kazi wake unategemea jinsi wanavyo ongozwa kwa kiasi kikubwa zaidi. Hivyo wakifanya vizuri utajua unawaongoza vizuri, na wakifanya vibaya utajua unawaongoza vibaya. Na hata kama utendaji wao mbaya sio sababu ya uongozi wako, ukiwasaidia kuboresha utendaji wao utakuwa umefanya kazi nzuri..

Kumbuka ulipotoka

Hapo zamani za kale na wewe ulikuwa ni kijana ukitafuta fursa, na mtu akakupatia nafasi. Na wewe fanya hivyo. Kama wewe bado unaweza kujikuza kitaaluma, nini kinamzuia mhitimu. Hivyo achana na mitazamo isiyo ya kweli, kuajiri mhitimu kuna faida nyingi kuliko hasara, faida ambazo unaweza usizipate kwa kuajiri mtu mwenye uzoefu.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.