Njia 5 za Kuendelea Kuwasiliana na Bosi Wako wa Zamani

  | 3 min read
0
Comments
1535
wasiliana na bosi wa zamani

Bosi wako wa zamani hafai kubaki katika historia yako tu. Katika kipindi hiki ambacho kupata fursa mpya inategemea uhusiano na mapendekezo kutoka kwa watu wenye sifa nzuri, kuwa katika mawasiliano na bosi wako wa zamani ni muhimu. Anajuana na watu wengi,  anajua historia yako ya kazi na anaweza kuthibitisha ujuzi na uwezo wa kazi zako wakati unahitaji utambulisho sehemu fulani. Unaweza kuonekana una ubinafsi ikiwa utakaa kimya muda mrefu sana kisha kuja kumtafuta kuomba msaada. Ni sawa na kumtafuta mtu wakati wa shida tu.

Ingawa ni muhimu kuendelea kuwasiliana, unahitaji kuwa mwaangalifu katika hatua zako za kuwasiliana na mwajiri wako wa zamani ili kuepuka kutoelewana. Hizi ni njia muhimu za kuendelea kuwasiliana nae:

1. Tuma Kadi Wakati wa Likizo na Siku Muhimu

send holiday card

Kadi ni njia muhimu ya kuonyesha kuwa unajali na kumkumbuka mtu. Chukua muda wako kuandaa zawadi au kadi kwa Bosi wako wa zamani kumtakia ‘Heri ya Siku ya Kuzaliwa’ au ‘Heri ya Mwaka Mpya’ japo mara moja kwa mwaka. Jaribu kutuma kadi isiyoegemea upande wowote kidini ikiwa hujui kuhusu dini yake na hakikisha kuweka ujumbe wako wazi ili kuepuka kutokuelewana.

2. Ungana Nao katika Mitandao ya Kijamii

Mitandao ya kijamii ni njia rahisi zaidi kuwasiliana na bosi wako wa zamani. Tafuta mtandao sahihi unaofaa kuwaunganisha na tumia mahusiano ya kawaida na ya kitaaluma tu kuwasiliana. Firikia sana juu ya aina ya uhusiano uliokua nao kabla ya kuondoka mahali pako pa kazi. Hii itakusaidia kujua mtandao sahihi wa kuungana nae. Ikiwa baadhi ya mitandao kama vile Facebook na Instagram inaonekana kuwa ni ya kibinafsi zaidi, fikiria kuungana nae kwenye mitandao ya kitaaluma zaidi kama LinkedIn.

3. Wafahamishe kuhusu Matukio Yako Muhimu ya Maisha

give updates on your major life event

Sio wazo baya kumshukuru bosi wako wa zamani kwa lolote lililopelekea wewe kufika hapo ulipo. Mpigie simu baadhi ya nyakati kumjulishe kwamba umepandishwa cheo, unahamia mkoa / nchi nyingine kikazi, au unabadilisha jina na anwani yako. Unaweza pia ukampelekea mwaliko ili ahudhurie kwenye matukio yako muhimu ya maisha kama vile harusi au utoaji shukrani kila mwaka. Hii ni njia nzuri ya kuwashukuru na inaweza kuwa kiungo muhimu kati ya fursa zako kitaaluma za siku za baadae.

4. Mtumie Makala Muhimu na Zinazowafaa

Unaweza kumfanya bosi wako wa zamani akuone unamjali na kumkumbuka kwa kumtumia makala na machapisho muhimu utakayokutana nayo mtandaoni. Mtumie barua pepe yenye kiungo (link) yenye makala nzuri, huku ukimwandikia ujumbe mfupi kama vile ‘Habari Bosi, nadhani utavutiwa sana na makala hii.’ Kumbuka kufanya barua pepe yako iwe fupi hakikisha kuna uwiano sahihi kati ya makala yako na umuhimu wako wa kutaka kuwasiliana nae.

5. Tembelea Ofisi ya Zamani au Panga Kukutana Nae

visit old office or plan meet-up

Ikiwa kazi yako mpya ulipata katika mji huo huo, unaweza kumualika bosi wako wa zamani kwa chakula cha mchana au kikombe cha kahawa katika mgahawa mara moja moja kwa mwaka. Ni njia nzuri sana ya kuongea mengi na kupata ushauri muhimu wa kazi zako. Ikiwa kazi yako mpya iko katika mkoa tofauti, siku ukipata nafasi ya kutembelea mkoa ulipo ofisi yako ya zamani, basi tafuta nafasi kupita kusalimia. Ni nafasi nzuri pia ya kukutana na wafanyakazi wenzako wa zamani, na kubadilishana mengi.

 

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media