Zawadi kwa Mwajiriwa: Njia za Kuwapongeza Wafanyakazi Wako

  | 5 min read
0
Comments
1273
Zawadi kwa Mwajiriwa: Mkakati na Njia za Kutambua Wafanyakazi Wako

Kuwazawadia wafanyakazi wenye utendaji mzuri inamaanisha kutambua mchango wao katika kampuni. Wafanyakazi wako watafurahia maoni juu ya kama wamefanya vizuri au la, ili waweze kuboresha utendaji wao. Kutambua mchango wa mfanyakazi wako unaweza kufanywa kwa ishara au au kauli rahisi tu. Ukimwonyesha manyakazi wako unatambua mchango wake, basi ni njia rahisi lakini yenye ufanisi mkubwa wa kuwafanya wafanyakazi wako kuwa waaminifu na wenye ari ya kazi. Utafiti unaonyesha kwamba, mashirika ambayo ‘Husema Ahsante‘ mara kwa mara wafanyakazi wake hufanya vizuri zaidi ya yale ambayo hawashukuru wafanyakai wao.

Tafiti pia inaonyesha kwamba, ili kuboresha utendaji wa shirika na kuhamasisha wafanyakazi wako, unahitaji kufanya yafuatayo;

establish trust among employees

  1. Kukuza imani miongoni ya wafanyakazi wako kwamba zawadi hizi utakazotoa kwa wafanyakazi zinahusinana na mafanikio ya shirika. Mfano, utendaji mzuri wa mfanyakazi kwenye mahusiano mazuri na wateja, uwezo binafsi wa kutatua changamoto muhimu au uwezo wa kumsaidia mfanyakazi mwenzake.  
  2. Kutoa mawasiliano ya wazi juu ya utendaji mzuri kwa wanachama wote wa timu
  3. Kuweka njia rahisi kwa wafanyakazi wako kuchangia moja kwa moja utendaji wa shirika.
  4. Kuunda fursa kwa kila mfanyakazi kujifunza jinsi ya kuchangia katika mafanikio ya shirika na jinsi ya kupima utendaji wao.

Kuunda Mfumo Thabiti wa Kuwazawadia

Ili kuonyesha kuwakubali na kuwazawadia watumishi wako, unahitaji kuzingatia yafuatayo:

  1. Wape Tuzo Wafanyakazi Wako kulingana na Utendaji na Matokeo

Ikiwa wafanyakazi wako wamefanya vizuri, mfano kuchukua hatua nzuri kutatua tatizo fulani au kwenda zaidi na zaidi katika kuwasaidia wateja, wanahitaji kutambuliwa. Hii itawahamasisha wafanyakazi wako kwenda maili ya ziada wakati wa kufanya kazi zao.

2. Wafanye Wapongezane Wao Kwa Wao

Implement a Peer-to-Peer Recognition

Pili, unahitaji kutekeleza mkakati ambao wafanyakazi wataweza kutambua mafanikio ya wenzao moja kwa moja, na papo hapo. Hii inaweza kufanyika kupitia ubao wa ndani ya ofisi au tovuti ya kampuni. Ikifika mwisho wa kila mwezi mfanyakazi ambae atakuwa amepongezwa na kutambuliwa zaidi kutoka kwa wenzao anapata kadi ya tuzo au zawadi.

3. Fanya Upongezaji Uwe Rahisi na  wa Mara kwa mara

Utaratibu wa kutambua na kuwapongeza wafanyakazi wako unapaswa kuwa rahisi na wa muda mfupi ili kuepuka kuchukua muda wa wafanyakazi. Unaweza kutumia kadi au fomu ya wafanyakazi ili kutaja kwa nini wanahisi mtu fulani anapaswa kutambuliwa n akupongezwa kwa uchapaji kazi mzuri.

Njia za Kuwazawadia Wafanyakazi Bila Gharama Kubwa

Kuwazawadia wafanyakazi wako haipaswi kuwa tukio starehe au gharama kubwa. Ikiwa kampuni iko katika wakati mgumu kifedha, si sababu ya kuacha kutambua wafanyakazi wako. Unahitaji kutafuta njia ya kutambua na kuwazawadia wafanyakazi wako kwa kazi nzuri walizofanya. Hizi ni njia za kuwazawadia kwa gharama ndogo:

1. Anzisha Mfumo wa ‘Ukuta wa Watu Maarufu’

Establish A ‘Wall of Fame’ System

Unda ukuta wa watu maarufu (Wall of Fame) ambao utajumuisha nukuu au picha za wateja wanapo wapongeza wafanyakazi wako. Pia unaweza kubandika vitu kama chati na maendeleo mazuri ya utendaji kwa mwezi husika, au pongezi za wafanyakazi kwenda kwa mfanyakazi fulani. Unaweza kutumia picha ya mfanyakazi huyo wa mwezi pamoja na maelezo juu ya kile alichofanya hadi kupongezwa.

2. Toka Nao Kupata Mlo wa Pamoja

Mkakati mwingine ni kutoka na mfanyakazi anayestahili kwa chakula cha mchana na kutumia wakati huu ili ujue zaidi kuhusu maisha yao. Hakikisha huongelei mada zinazohusiana na kazi na badala yake kuzungumza juu ya maslahi yao na vivutio vyoa nje ya kazi.

3. Kutoa Hati za Mafanikio

Provide Certificates of Achievements

Unaweza pia kumkabidhi mfanyakazi wako hati ili kumshukuru kwa mafanikio fulani. Hii inaonyesha kwamba mfanyakazi wako amepiga hatua muhimu katika kazi. Kwa mfano, unaweza kumpa kazi mfanyakazi wako hati ya mafanikio kwa kufikia lengo maalum la mauzo ya kampuni au mafanikio ya maendeleo ya kibinafsi.

4. Wape Masaa Ya Ziada 

Chagua pia kutambua mfanyakazi anayefanya vizuri kwa kuwapa kipaumbele na marupurupu kama vile kufika kazini baada ya mda wa kazi kuanza / kuondoka mapema zaidi kazini, au mapumziko ya muda mrefu ya chakula cha mchana. Pia unaweza kuchagua kuruhusu mfanyakazi mwenye kustahili kufanya kazi akiwa nyumbani wakati wa matukio muhimu ya maisha yao kama vile msimu wa kurudisha watoto shule, siku ya kuadhimisha ndoa zao na mengine.

5. Jumuika Nao Kusherekea Siku Zao Muhimu

Njia nyingine ya kutambua na kuwazawadia wafanyakazi wako ni kwa kujumuila nao kusherehekea siku zao za kuzaliwa, kuzaliwa kwa watoto, harusi, kuhitimu na vingine. Kusanya timu yako pamoja kwa ajili ya keki na kujichanganya nao itafanya wafanyakazi wako kuhisi kupendwa na kuthaminiwa.

6. Shukuru Familia Yote ya Mfanyakazi wako

Zaidi ya hayo, unaweza pia kukaribisha familia ya mfanyakazi wako kujumuika katika  sherehe za kampuni. Tumia fursa hii kuzungumza nao kuhusu kiasi gani unavyothamini mchango wa ndugu yao. Unaweza pia kutuma kadi na barua kwa familia ya mfanyakazi wako, kuwaambia kwa nini mpendwa wao ni muhimu kwa ukuaji wa kampuni.

7. Waalike kwenye Kikao Kuwashukuru

Invite Them for a ‘Thank You’ Meeting

Wakati mfanyakazi wako anafanya jambo la kufurahisha, usisite kuchukua dakika moja tu na kumshukuru mbele ya wafanyakazi wenzake kwa mafaniki yake. Ita wafanyakazi wengine wakusanyike pamoja kisha tumia wasaa huu kumshukuru mbele ya wafanyakazi wengine na kutaja sababu maalum kwa nini unampongeza.

Sababu ya kuwazawadia wafanyakazi wako ni kuwahamasisha na kuwapa sababu za msingi za kuendelea kuboresha utendaji wao. Hivyo, wakati mwingine watakapofanya jambo jema, chukua muda wako na kutambua mchango wao. Hii itawafanya wajisikie kuthaminiwa. Tuambie mawazo yako katika hili kwenye sehemu ya maoni hapa chini.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media