Job Summary

Tunatafuta mtu anaekidhi vigezo vya kuchukua nafasi ya Mhasibu.

  • Minimum Qualification: Bachelor
  • Experience Level: Executive level
  • Experience Length: 3 years

Job Description

MAJUKUMU YA KAZI

i. Kusimamia utendaji wa kazi katika Idara ya Uhasibu;

ii. Kuandaa hesabu za mwaka na kuhakikisha zinawakilishwa kwa mkaguzi wa nje(COASCO) kulingana na taratibu za ukaguzi;

iii. Kusimamia watumishi wote wanaoshughulika na kazi za fedha za Chama;

iv. Kusimamia utunzaji wa mapato ya Chama na kuhakikisha matumizi yanaendana na yale yaliyoidhinishwa;

v. Kusimamia utayarishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka na kuwasilisha bajeti kwa Meneja wa Chama;

vi. Kutoa taarifa ya fedha za Chama kila mwezi, kila baada ya miezi mitatu na mwisho wa mwaka kwa Meneja;

vii. Kutoa ushauri mara kwa mara kwa Meneja kuhusu hali ya mapato na matumizi;

viii. Kutayarisha na kutoa malipo yaliyoidhinishwa na mamlaka ya fedha kulingana na taratibu za fedha;

ix. Kufanya malinganisho ya miamala ya leja kuu na hesabu za benki kila mwezi;

x. Kubuni mbinu za kupata mapato ya ziada kwa Chama;

xi. Kushirikiana na wakaguzi wa hesabu wa ndani na nje katika kukamilisha ukaguzi

wa hesabu za Chama;

xii. Kutimiza majukumu mengine atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi;


SIFA ZA MWOMBAJI

i. Awe na umri wa miaka 30 na kuendelea;

ii. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu (3) wa kufanya kazi za uhasibu kwenye taasisi yoyote inayotambulika au katika Chama cha Ushirika

iii. Awe na Shahada ya Uhasibu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na awe na CPA (T)

iv. Awe na ujuzi wa kutumia Computer hasa Tally programu

v. Awe na sifa ya uadilifu;

vi. Awe hajawahi kufukuzwa kazi kwa tuhuma za upotevu wa fedha.

MSHAHARA

Kiwango cha mshahara (…………….ni makubaliano)


MASHARTI YA JUMLA KWA NAFASI YA KAZI

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania

ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa

iii. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika, Barua iliyoandikwa kwa mkono na kusainia.

iv. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika, Vyeti vya kitaaluma (Professional Certificate from respective Board)

v. “Testmonials” “Provisional Results”, “Statement of results” hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA

vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA, na NACTE)

vii. Mwombaji atakayeitwa kwenye usaili aje na vyeti halisi siku ya usaili

viii. Mwombaji atajigharamia mwenyewe wakati wa usaili

ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

x. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

xi. Maombi yote yatumwe kupitia anuani tajwa hapa chini

xii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 10th February 2020

MWENYEKITI WA BODI

CHAWAKIM COOPERATIVE SOCIETY LTD

S.L.P 30871,

KIBAHA TANZANIA

E mail: chawakim@yahoo.com

Share Job Post

Log In to apply now

Dar es Salaam
| Full Time |
TSh Confidential
1mo
Dar es Salaam
| Full Time |
TSh Confidential
1mo
Dar es Salaam
| Full Time |
TSh Confidential
1mo