New

Job Summary

Mkurugenzi mtendaji wa Bwipa Company Limited anatangaza nafasi 1 ya kazi ya Dereva wa gari la kampuni.

  • Minimum Qualification: Certificate
  • Experience Level: Mid level
  • Experience Length: 2 years

Job Description

Bwipa Company Limited (BCL) ni kampuni iliyosajiliwa kwa mjibu wa sheria na taratibu za Tanzania na kupata vibari vyote vya kufanya shughuli mbali mbali zikiwemo:- Usafi majumambani, maofisini na maeneo tofauti tofauti ya biashara(General Cleaning Service), Kusugua na kung'arisha marumaru (Tiles Scrubbing & Polishing), Kusafisha Kapeti na Sofa (Carpet & Sofa Cleaning), Kupuliza dawa ya kuua wadudu warukao na watambaao (Fumigation), Kutengeneza/kuhudumia viunga na mazingira kuzunguka nyumba/ofisi(Gardening), Kufua (Laundry), Wasichana wa kazi majumbani kwa kutwa (Maids Service), Kuhamisha mzigo majumbani/maofisi (Moving Service) na Kuosha magari (Mobile Car Wash).


Mkurugenzi mtendaji wa Bwipa Company Limited anatangaza nafasi 1 ya kazi ya Dereva wa gari la kampuni. Aidha,Dereva atakae ajiriwa atafanya kazi ofisi kuu ya BCL iliyopo Dodoma. Hivyo maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi ya kazi 1 yanakaribishwa.

 

 

MAJUKUMU YA KAZI

I.      Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,

II.      Kuwapeleka wafanyakazi maeneo mbalimbali kwenye shughuli za kampuni,

III.       Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,

IV.      Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali za kampuni,

V.      Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (Log book),

VI.      Kufanya usafi wa gari,

VII.      Kufanya kazi nyingine kadri anavyoelekezwa na Msimamizi wake.

 


SIFA ZA MWOMBAJI

I.      Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri kati ya miaka 25-45.

II.      Awe na leseni ya Daraja la D, C3, C2, C1 au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka bila kusababisha ajali.

III.      Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari yanayotolewa na Chuo cha

Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. IV.      Awe na uwezo wa kuendesha gari MANUAL.

V.      Waombaji wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza. VI.      Aweze kuzungumza na kuandika Kiswahili au Kingereza kwa ufasaha.

 


MASHARITI YA JUMLA KWA WAOMBAJI.

Mwombaji aambatanishe barua ya maombi ya kazi, maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika, nakala ya vyeti vyake vyote vya elimu na mafunzo ya udereva, barua ya mwenyekiti wa mtaa ya utambulisho kuwa yeye ni mkazi wa mtaa husika, nakala ya cheti cha kuzaliwa pamoja na passport size moja.

 

 

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Maombi  ya  kazi  yatumwe  kwa  Mkurugenzi  Mtendaji  BWIPA  COMPANY  LIMITED  S.L.P  2434, DODOMA kwa email:  cbwipa@gmail.com  au maombi yaletwe moja kwa moja ofisi za BWIPA COMPANY LIMITED zilizopo mtaa wa Makole barabara ya Dodoma Inn. Mwisho wa kupokea maombi ya kazi ni tarehe 31/10/2020 saa 11:00 jioni.

Important Safety Tips

1. Do not make any payment without confirming with the BrighterMonday Customer Support Team. 2. If you think this advert is not genuine, please report it via the Report Job link below.

Share Job Post

Log In to apply now

Activate Notifications Stay productive - get the latest updates on Jobs & News
Activate
Deactivate Notifications Stop receiving the latest updates on Jobs & News
Deactivate
Dar es Salaam
| Full Time |
TSh Confidential
1w
Rest of Tanzania
| Full Time |
TSh Confidential
3d